kevin-hart-press-photo-2014-1409830783-article-0

 Mwanamuziki Diamond Platnumz yupo nchini Marekani ambapo amekwenda kwaajili ya kufanya tamasha la muziki Los Angeles lakini pia kutengeneza video ya wimbo wake alioimba na mwanamuziki NeYo wa Marekani ambao bado haujatoka.

Akiwa nchini Marekani, Diamond Platnumz ameweka video kwenye akaunti yake ya Instagram ikimuonyesha akiwa na mchekeshaji maarufu kutoka nchini humo, Klevin Hart.

Mara kadhaa Diamond amekuwa akionekana na watu maarufu, na yeye alisema kuwa anapopata wasaa na watu hawa, huakikisha anafanya kitu kikubwa chenye faida. Swali linabaki, Je! tutegemee chcochote kati ya Diamond Platnumz na Klevin Hart?

Tazama video hii hapa chini.