Q Chief amethibitisha nyumba yake kuvamiwa na majambazi na wamefanikiwa kuiba baadhi ya vitu vilivyomo ndani ikiwemo laptop iliyokuwa na baadhi ya colabo zake.
Q-Chief.jpg.pagespeed.ce.hup1vLSgDZ
Akiongea na Kituo kimoja cha radio , muimbaji huyo amedai kuwa thamani ya vitu vyake vilivyoibiwa ni kama milioni mbili au tatu.
“Watumishi wa shetani wameamua kufanya kitu cha kihistoria, siku zote wanarukaruka mmoja wawili tunapigiza nao kelele wanaondoka lakini this time wamekuja watu kama sita, saba au nane. Wamekuja na mapanga, wamekuja na mafokolisti yale ya kufungua, wamekuja na gari moja nje sasa sijui walikuwa wanataka kubeba kila kitu?,” ameuliza Q Chief.

 

Advertisements