bills-602x375

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye ndiye mmiliki wa jengo la Club Bilicanas lililopo Post jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa waidawa sugu ambapo hawajilipia pango na walipewa notisi inayofikia mwisho mwezi huu.

Mchechu amesema mbali na Mbowe kuna taasisi nyingine za watu binafsi na za Serikali ambazo nazo zinadaiwa malimbikizo ya kodi. Ameeleza kuwa kama hadi mwisho wa notisi watakuwa hawajalipa malimbikizo hayo, wataondolewa katika nyumba hizo wanazozitumia bila kujali nani ni nani.

Advertisements