harmo
Rajabu Abdul, maarufu kama Harmonize, msanii wa kizazi kipya anayetokea kundi la Wasafi lililopochini ya usimamizi wa Menejimenti ya Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika studio za Wasafi Record Lebal, amejichora tatoo kwenye mkono yenye sura za watu wawili muhimu sana maishani mwake, na hiyo ni kwa mujibu wake.

Katika tatoo yake, sura ya kwanza inayoonekana ni ya mama yake mzazi, na kusema haya kumhusu ‘Mama yangu ni zaidi ya kila kitu maishani mwangu ❤❤❤#Habiba wangu nakuombea uishi miaka mingi uje kuvuna ulichokipanda ….🙏🙏🙏’.

Sura ya pili ni ya msanii Diamond Platnumz, huku yeye Harmonize akimuita kwa jina la Simba.

WhatsApp Image 2016-08-23 at 12.25.23 AM (1) WhatsApp Image 2016-08-23 at 12.25.23 AM