Diamond Platnumz
Diamond Platnumz amefanikiwa kile ambacho hakuna msanii wa Tanzania amewahi kufanikiwa huku kukiwa na wasanii wachache tu wa Afrika wamekifikia – kuingia kwenye playlist ya kituo cha redio cha BBC Radio 1Xtra.Imefahamika kupitia Playlist ya wiki nzima ya kituo hicho maarufu cha redio iliyotolewa Ijumaa hii, August 12. Diamond na P-Square, wanaungana na Wizkid kama wasanii pekee wa Afrika waliopo kwenye playlist ya kituo hicho.

Hiyo ina maana kuwa Kidogo itakuwepo kwenye mzunguko wa nyimbo za kila siku zinazochezwa kwenye kituo hicho cha redio kwa wiki nzima na kuna uwezekano wa kuendelea zaidi na kuongezeka rotation yake.

Advertisements