Msanii wa Miduara AT amemporomoshea matusi mazito msanii mwenzie wa Bongo Flava Peter Msechu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Katika post hiyo ambayo imeambatana na Picha ya Msechu, AT amemtupia lawama msanii huyo akidai amekuwa na tabia ya kumsema hovyo bila kujua chanzo chake.

“Mvuto Sifuri Bikaka @peter_msechu Nene km Lori Hivi kuongelea wembamba wangu unalipwa sitaki shobo km lakufanya huna jikate minyama yako ujichome mishkaki usi nitekenye mdomo ukataka niongee Tumbo Tumbo km Umeficha Kobe wewe nipotezee usilazimishe mimi niwe karibu na wewe sina shida ya kukuazima tumbo nende nalo harusini Mifulana km Turubali za Msimbani Babu kaa mbali na mimi kwani hivi na wewe ni msanii wanchi hii au Muuza kufia za Oliva Mtukuzi? Pyuuuuuuuuuuuuu ukiona nipo kimnya ujue sihitaji varangati na mtu kiki zime adimika huna utakapopatia usinione Mwembamba ingia 18 uhadithie wenzio Mr Machupi ya kushonesha.!!” Ameandika AT.

Advertisements