256636_10150278492914575_675834574_9243480_5726081_o
Baada ya miezi kadhaa ya kutoelewana na kusababisha kuvunjika kwa kundi la P-Square sasa, Peter na Paul Okoye wameanza kurekodi kazi mpya.
Mwezi Julai mwaka huu member wa kundi hilo Peter Okoye aliandika ujumbe kwenye Instagram akiwaomba msamaha mashabiki wao kwa kuvunjika kwa kundi hilo lakini aliwaahidi kuwa P-Square linarudi tena na alitangaza kumrejesha kaka yao, Jude Okoye kama meneja wao.
Kupitia akaunti ya Instagram, Peter ameandika ujumbe unaoonyesha kuwa kuna kitu kipya anarekodi studio na ndugu yake Paul.

Something new Cooking in da kitchen and about to come out! From us! You already know it’s P2 baby!!! #KoolestDudes


Kurudi upya kwa kundi hilo ni ndoto ya kila shabiki wa muziki Afrika kutokana na heshima kubwa waliojitengenezea kipindi walipokuwa pamoja. Muda ndio utaongea tusubiri tuone

Advertisements