Msanii wa muziki, Shetta amemuweka wazi kijana anayemtuhumu kutapeli watu katika mitandao ya kijamii kwa kutumia jana lake.
13895393_1058672627519385_8263238224076065565_n
Shetta akiwa na kijana anayemtuhumu

Rapper huyo amewataadharisha mashabiki wake pamoja na wadau mbalimbali kuwa makini na watu hao.

“Kuna huyu jamaa inasemekana anatumia akaunti tofauti tofauti facebook na kwenye mitandao mengine kutapeli watu,” aliandika Shetta katika mtandao wa facebook.

Aliongeza, “Na hii picha anaitumia sanaaa nimepata malalamiko mengi juu yake. Alikuja kwenye Instagram Party kama shabiki na akaomba kupiga picha hii miaka miwili iliyopita kiukweli simjui ila napata malalamiko kwa watu kuwa yeye ndio anatapeli na hutumia picha zangu kama kigezo kila sehemu. Nasisitiza tena kuweni makini na mitandao na nyie mnaotapeli watu jela inawaita,”

Wasanii wengi pamoja na watu maarufu wamekuwa wakilalamika watu kutumia majina yao katika kitandao ya kijamii kwa ajili ya kutapeli watu.

Advertisements