Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva anashikiriwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru). Taarifa zilizothibitishwa na Polisi ni kuwa Rais wa Simba bwana Evans ameshikiriwa na wenzake ambao hawakutajwa kwa sababu zilizotajwa kuwa ni kulinda taratibu za uchunguzi.Taarifa zinaelezwa kuwa Takukuru wanamshikilia Aveva kwa tuhuma za rushwa ingawa haijaelezwa ni tuhuma zipi. Habari za uhakika zinaeleza, Aveva amekamatwa jana na amelala katika moja ya vituo vya polisi jijini Dar es Salaam. Kwa taarifa zaidi endelea kutufuatilia

 

Advertisements