Baada ya video ya wimbo wake wa ‘Jike Shupa’ kufanya vizuri,msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nuh Mziwanda amaesema kuwa sasa atajitahidi kutoa vibao ‘vikali’ ili jina lake lipase umaarufu ndani na nje ya nchi.

Mziwanda amesema kuwa mipango yake ni kutumia vyema kipaji alichonacho ili kutimiza lengo lake la kuwa msanii wa kimataifa.

“Nina uhakika nitaendela kimuziki kwa kutumia kipaji changu na siyo ‘skendo’ za mapenzi kama ilivyokuwa miaka ya yuma,zilitaka kunupoteza,nimeshtuka na sasa niko kikazi zaidi,”alisema Mziwanda.

Alisema kuwa kuna baadhi ya watu walitegemea kwamba ameshindwa kufanya shughuli za muziki baada yake ameanza kurejea kwenye ushindani.

“Skendo siku hizi hazina mango,mashabiki wanataka kusikia kazi tu na kwa sababu msanii akiwa juu ya jukwaani anatakiwa kuonyesha ubora wake,” alisema ambaye amemshirikisha Ali Kiba katika wimbo wake wa Jije Shupa.

Advertisements