Mwana FA unaoa lini? Miaka takriban kadhaa iliyopita, hili ni swali lililokuwa likimkera sana Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA. Jibu lake ‘Bado nipo nipo’ sana liligeuka kuwa jibu la vijana wengi hapa Tanzania ambao suala la kuoa halina nafasi vichwani mwao.

wp-1466108008056.jpeg

Lakini wahenga walisema hakuna hali inayodumu daima. Juni 5 mwaka 2016, Mwana FA alifunga ndoa na mchumba wake wa miaka mingi aliyebahatika kuzaa naye mtoto wa kike aitwaye Maleeka.

Sikiliza makala hiyo kuwasikia maswahiba wake Hermy B na Ommy Dimpoz wakizungumzia kwa undani kuhusiana na uamuzi huo wa FA.

Advertisements