selebobo
Oku Chigozie ‘Selebobo’
MREMBO kutoka Bongo asiyekaukiwa matukio, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa msanii ambaye pia ni produza kutoka Nigeria,

Oku Chigozie ‘Selebobo’ ameamua kumkamatia moja kwa moja kikazi ili kuhakikisha anasonga mbele na kuufikisha muziki wake kimataifa zaidi.

shilole (1)
Zuwena Mohammed ‘Shilole’
Akichonga na gazeti hili Shilole akiwa katika maandalizi yake ya mwishomwisho ya safari kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki alisema mbele ya prodyuza huyo anategemea kuwa msanii mkubwa na akitoka Afrika Kusini ataelekea Nigeria kwa ajili ya maongezi zaidi na msanii huyo ikiwemo kufanya kichupa cha kolabo waliyofanya miezi michache iliyopita.
Selebobo-Pic
“Selebobo ameamua kufanya kazi na mimi moja kwa moja, nategemea atanifikisha mbali maana kama unakumbuka ndiye aliyemtoa Yemi Alade na wasanii wengi wenye majina makubwa Nigeria kwa sasa,” alisema Shilole.
Advertisements