Rapper Cyrill Kamikaze baada ya kuachia wimbo ‘Cheza Kidogo’ ambao amemshirikisha Raymond wa WCB na baadae uongozi wa WCB kuitaa kazi hiyo, Cyrill amefunguka ya moyoni.

cyrill-1

Kupitia ukurasa wa Instagram, Cyrill ameandika:

Daah hii imetaka kunisikitisha kidogo hasa kutoka kwa Manager huyu wa WCB kusema wanaikana ngoma yangu wakidai kuwa msanii wao hakushiriki .. Sasa kinachoni shangaza WCB imekua ni group ambalo msanii akiingia hata kama ana historia nyuma ifutike yani kama ana kua mtu mpya au msanii mpya vile na kupelekea kazi ambazo zimefanywa na msanii wao kabla zisitambulike.. Mbona jana nimehojiwa nimeongea vizuri kuwa nimefanya nae before hajaenda WCB na siku mtaja hata kama Raymond WCB? hata kwenye post yangu ya nyuma instagram sijamtaja,Seriously so inamaana huu huu mziki WCB kwa mujibu wa manager wanataka tuione kama UFALME fulani vile kuingia kwamba hakuna kinachofanyika bila wao?, hapana mashabiki tu wameweza ku support na kufanya hilo group na wasanii wa humo kuwa hapo walipo,kama Manager usivimbe kichwa nakuona kama umeshamaliza kila kitu haya ni maisha tu na kwa step mliofika wengi tumekua tukifurahi ila kama hata hili la ngoma tena ambayo sijataja WCB ume mind hizo ni chuki na kutopenda maendeleo ya mtu mwingine so mnataka mbaki nyie tu right? Well personally i dont really care labda kama unadhani utaniyumbisha no no i have been here and i will be here just doing my game sina haja ya competition bro.

Advertisements