Ukimya wa Akil The Brain, moja ya watayarishaji mahiri nchini na mwanzilishi wa Bongo Bhangra ulitokana na masahibu yaliyotokana na mke wake wa pili, imebainika.

12935158_208273772881309_1384013627_n

Akil ameiambia Bongo5 kuwa alikaa kimya kwa sababu baada ya kufanya vizuri kwenye muziki alipagawa kwenye penzi na binti aliyeamua kumuoa kama mke wake wa pili.
Anadai kuwa baada ya kumuoa binti huyo alianza kumletea sheria zilizomgharimu kwenye muziki wake.

Anasema alikuwa hataki pia aendelee kuiona familia yake ya mke mkubwa na watoto kwa ujumla jambo ambalo Akil alimsikiliza kutekeleza kwa kuwa alikuwa ameshazama kwenye mapenzi na mke wa pili.

“Kuna wakati nilikuwa najifungia nalia tu maana nakuwa nimewakumbuka wanangu na mke wangu na inanibidi nijiibe niende kuwaona lakini marehemu mama yangu aliniusia sana juu ya mke wangu mdogo na mbaya zaidi mke mdogo alikuwa hataki hata nifanye video na mwanamke. Tukienda kwenye show hanipi uhuru wa kucheza hata na stage shows, nikifanya mziki ananuna nuna mwisho nikaona naelekea pabaya na mpaka naachana naye nilikuwa sina hata shilingi kumi mfukoni,” amesema Akil.
“Niliamua kurudi kwa mke wangu mkubwa na kuanza maisha mapya.

Akil amedai kuwa katika kipindi hicho alipata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ambao ulimfanya kukaa mbali kidogo na game ili apate ahueni ambayo inaweza kumfanya kurejea tena.
Anasema kwa sasa anashukuru Mungu anaendelea vyema na amerudi kwenye Bongo Banghra na wimbo wake Popo aliomshirikisha Shilole.

IMG-20160501-WA0000

Wimbo huo umeandikwa na rapper Baghdad kuanzia melody na mashairi huku Akil akiutayarisha mwenyewe.

Advertisements