Msanii wa filamu, Baby Joseph Madaha, ameibuka na kudai kwa sasa ameamua kutulia katika ndoa yake na Mwarabu wa Dubai ambaye hakutaka kumtaja jina.
Baby Madaha

Muimbaji huyo ambaye yupo mbioni kuachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Corazon’, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa kwa sasa maisha yake ni Tanzania na Dubai.

“Kwa sasa ninaishi nchi mbili, nipo Tanzania na pia nina makazi yangu mapya huko Dubai, nimeolewa na Mwarabu na nimetulia kwenye ndoa yangu najiachia kwangu, ahaaaa!” alijibu kisha akamalizia kwa kicheko.

Madaha amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio ya video yake mpya ambayo ameshoot Dubai.

Advertisements