Harmonize amedai kuwa hamkopi bosi wake Diamond katika uimbaji wake.

maxresdefault

Hitmaker huyo wa Bado amedai kuwa Diamond ana utambulisho wake hasa katika nyimbo za kulalamika na kwamba huu ni muda sasa watu wakaanza kuwatofautisha.

“Ukimzungumzia Diamond unamzungumzia mtu ambaye ana melody za malalamiko ambazo zimeganda katika vichwa vya watu wengi, kwahiyo nikiimba malalamiko lazima watu watakufafanisha,” Harmonize aliiambia 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Lakini huu ndio wakati mzuri wa kutambua huyu ni Harmonize, huyu ni Diamond,” ameongeza.

Harmonize alimshirikisha bosi wake huyo kwenye wimbo wake Bado unaofanya vizuri kwa sasa.

Advertisements