Nyota wa muziki wa Pop Prince hakuwacha wasia ,dadaake amefichua katika stakhabadhi za mahakama.

Nakala zilizowasilishwa katika mahakama ya jimbo la Minnesota zinaonyesha,Tyka Nelson ametoa ombi la mtu atakayesimamia mali ya nyota huyo.

Prince mwenye umri wa miaka 57 alipatikana amefariki katika lifti katika studio yake ndani ya makaazi ya Minneapolis,huko Minnesota Alhamisi iliopita.

Ukubwa wa mali yake haujulikani lakini unadaiwa kuwa dola milioni 27.

Nelson ni dadaake Prince aliyesalia na amesema katika nakala hizo kwamba hatua za haraka zinafaa kuchukuliwa ili kusimamia biashara za nduguye.

Nyimbo za Prince zimetewala chati za Uingereza wiki hii,huku mashabiki wanaomuomboleza wakinunua muziki wake huku ripota wa Hollywood akisema kuwa zaidi ya nyimbo milioni tatu za muziki wake pamoja na albamu zimenunuliwa nchini Marekani tangu kifo chake.

Advertisements