Tuzo maalum ya heshima kutoka Uholanzi kwa Van Gaal

https://i0.wp.com/i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/01/01/245B17A600000578-2893352-image-a-10_1420110267587.jpg

PICHA KWA HISANI YA EMPICS Sport

Manchester united ni kama haina bahati msimu huu kwani mpaka sasa bado haipo katika kiwango kizuri cha uchezaji na inakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.

Pamoja na kutokuwa na kiwango kizuri lakini bosi wa klabu hiyo Louis Van Gaal ameweza kuibuka mshindi katika tuzo maarufu ya Anton Geesink ambayom hutolewa nchini Uholanzi.

Tuzo hiyo maalum hutolewa kwa mtu, mji au kundi la watu lililofanya vema katika michezo mbalimbali.

Van Gaal ambaye kikosi chake cha Man united hakiko katika kiwango kizuri msimu huu amepewa tuzo hiyo baada ya Uholanzi kuonyesha kiwango bora na kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia nchini Brazil, mwaka jana

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.