Staa wa muziki Mheshimiwa Temba amezungumzia suala la yeye kubadilika na pia kubadili muziki wake kutokana na ngazi aliyofikia, ambapo amesema kuwa kwa upande wake hawezi kuishi maisha ya kuigiza na ambapo atakuwa anaidanganya jamii.

msanii wa kundi la TMK Wanaume Mh.Temba

Staa huyo ambaye hivi karibuni amekanusha ripoti zilizokuwa zimesambaa kuhusu yeye kuhusika katika kesi ya kutishia maisha, amesema kuwa chochote anachofanya na kile alichonacho ndicho ambacho kitaonekana na watu kutoka kwake na si zaidi.

Advertisements