Msanii wa muziki wa Rap duniani, Ludacris anatarajia kuachia album yake mpya iitwayo ‘Ludaversal’ March 31 mwaka huu.

Album hiyo mpya ya nyota wa filamu ya Fast and Furious kwa sasa Furous 7 itatoka katika wakati ambao Ludacris anatarajia kupata mtoto kutoka kwa mke wake kipenzi Eudoxie aliyefunga naye ndoa mwishoni mwa mwaka jana 2014.

‘Ludaversal’ ni album kali yenye nyimbo kama 18 zikiwepo “Good Lovin” aliomshirikisha Miguel, “Call Ya Bluff” na “Beast Mode” na imehusisha wasanii wakubwa kama Usher Raymond, David Banner, Big K.R.I.T, Miguel, Rick Ross na wengine.

Aidha album Ludaversal itakuwa ni mapinduzi mengine ya muziki wa Hip Hop duniani kutokana na ukali wa nyimbo zilizomo katika album hiyo.

Tazama orodha kamili ya nyimbo za album hiyo ya Ludacris hapa….

LUDAVERSAL TRACKS
1. “Ludaversal Intro”
2. “Grass Is Always Greener”
3. “Call Ya Bluff”
4. “Lyrical Healing”
5. “Beast Mode”
6. “Viagra Skit”
7. “Get Lit”
8. “Come and See Me Interlude”
9. “Come and See Me” (feat. Big K.R.I.T.)
10. “Good Lovin” (feat. Miguel)
11. “Ocean Skies” (feat. Monica)
12. “Not Long” (feat. Usher)
13. “Charge It to the Rap Game”
14. “This Has Been My World”

Deluxe Edition Tracks
15. “Money” (feat. Rick Ross)
16. “Problems” (feat. CeeLo Green)
17. “In My Life” (feat. John Legend)
18. “Burning Bridges” (feat. Jason Aldean)

Advertisements